NA
JUHUDI FELIX
KARAGWE
Watendaji wa halmashauri nchini
wametakiwa kusimamia vema miradi ya maendeleo na kuwa na uadilifu na
uwajibikaji kwa serikali iliyopo madarakani kwa ajili ya kuwahudumia wananchi
wake.
Agizo hilo limetolewa na mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe katika ziara ya
kukagua miradi ya maendeleo kwenye
wilaya ya Karagwe wakati akiongea na viongozi na watendaji wa
halmashauri hiyo.
Amesema kuwa endapo viongozi watasimamia
vema miradi ya maendeleo na kuongoza
wananchi kwa uadilifu ufanisi katika shughuli za maendeleo
utakuwepo na seikali iliyopo
madarakani itatimiza malengo yake ya kuwahudumia wananchi wa kada zote na
kuondoa manunguniko yaliyopo kwa sasa.
Aidha,Kanali Massawe ametoa agizo kwa wazazi na walezi kuwapeleka
watoto wao waliochaguliwa kujiunga na masomo ya sekondari ndani ya wiki moja ,kauli hii ameitoa baada
ya mkuu wa shule ya sekondari ya Ndama kusoma taarifa iliyobainisha mapungufu
wanafunzi 200 waliochaguliwa kujiunga na shule hiyo kati yao waliripoti
na kuanza masomo ni wanafunzi 40 tu.
Katika ziara hiyo mkuu wa Mkoa ameweza
kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo mradi wa ujenzi wa chuo cha ualimu Karagwe kilichopo kata ya Ihanda,mradi wa
umwagiliaji wa Mwisa Bujuruga,mradi wa maji wa Charuhanga,Shule ya sekondari ya
Kiruruma kukagua ujenzi wa bweni la wasichana,kutembelea Zahanati ya Omurusimbi
kwa ajili ya kukagua ukamilishaji wa ujenzi wake na kutembelea shirika la
Mavuno kukagua miradi mbalimbali ya shirika hilo.
No comments:
Post a Comment