Saturday, January 26, 2013

KARAGWE SECONDARI WASHEREKEA MAHAFALI YA 13 TANGU KUANZISHWA KWA MASOMO YA KIDATO CHA SITA.


NA
      JUHUDI  FELIX

KARAGWE
 

Wazazi na walezi wametakiwa  kutoa fursa sawa kwa watoto wao wa kike na wakiume ili kuwepo uwiana ulio sahihi katika kupata elimu na kuleta ushindani kwa jinsia zote bila ya upendeleo.

Wito huo umetolewa na Afisa elimu wa  wilaya wa shule za sekondari Hellen  Rugumira wakati akihutubia maafali ya kumi na tatu ya  kidato cha sita katika shule ya Karagwe sekondari. Amesema kuwa mara nyingi wazazi na walezi wanatoa fursa kwa watoto wa kiume kupumzika na kupata muda mwingi wa kupumzika na kujisomea huku watoto wa kike wakikosa muda wa kujisomea kwani ndio wanakuwa wasaidizi  wa shughuli za nyumbani warudipo nyumbani.


Rugumira pia amewataka wanafunzi kutumia vikao vyao halali vya shule kujadili na kuwasilisha changamoto zinazowakabili kwa uongozi na kuwataka wanafunzi kuongeza bidii katika masomo na kazi nyingine zo za kujitegemea.Pia ametoa  zawadi kwa shule hiyo ili kuongeza kasi ya ufaulu zawadi hiyo ya miongozo ya kufundishia kwa walimu.



Mwenyekiti  wa bodi wa shule hiyo Askofu mstaafu wa Diyosisi ya Karagwe Nelson   Kazoba akitoa nasaha zake kwa wazazi ,wanafunzi na wageni  waalikwa amesema kuwa kuna uvumi usiokuwa na ukweli ndani yake unaoenezwa mitaani na baadhi ya watu wasiipendea mema shule hiyo kuwa imeshuka  kitaaluma au haipokei wanafunzi na kuwatakuwa wasichafue shule hiyo na kuwataka watu na jamii kwa ujumla  kupata taarifa kwa vyanzo sahihi vya uongozi wa shule hiyo.



Naye kaimu mkuu  wa shule hiyo Donasian Rufulano akitoa neon la kuwaaga wahitimu hao amesema kuwa waendeleze malezi bora na ujuzi waliopata katika shule hiyo na wawe mfano bora kwa jamii. Ameongeza kuwa tayari  kuna chuo kutoka nchini Costarica kimetoa nafasi kwa wahitimu kujiunga nacho baada ya taratibu zote za usajili kukamilika na kuongeza kuwa fomu hizo zinapatikana katika ofisi ya taaluma shuleni hapo.

Kwa upande wao wahitimu  wakisoma risala kwa mgeni rasmi wamesemakuwa  wanapongeza uongozi wa shule kutatua tatizo la uhaba wa walimu haswa wa sayansi mbali na kupainisha pongezi  hizo wameuomba  uongozi wa shule hiyo  kuitisha  mikutano ya wazazi ,kutumia lugha ya kiingereza kwa shughuli zote za shule hata wakaomba pia iandaliwe sara kwa lugha hiyo ili waweze kuimudu na kuleta ufaulu kwa masomo yao.


No comments:

Post a Comment