Sunday, March 17, 2013
HII NDO BAJETI YA KARAGWE ILIYOPITISHWA
Na
Juhudi Felix
Karagwe
Halmashauri ya wilaya ya Karagwe imepitisha bajeti ya mapato na matumizi ya shilingi Billioni 50 katika kikao cha bajeti ya mwaka 2013hadi 2014.
Hayo yalibainishwa na mkurugenzi mtendaji wa Hlmashauri hiyo,Bosco Ndunguru wakati akisoma bajeti hiyo katika kikao cha baraza la madiwani kilichifanyika katika ukimbi wa vijana Rafiki Angaza wa wilaya hiyo.
Alisema Halmashauri hiyo katika bajeti ya mapato na matumizi imepitisha kiasi cha shiling Bilion hamsini milioni ishirini na sita laki tatu ishirini na saba elfu na na miambili tisini na nne na sente themanini.{50,263,227,294.80}
Ambazo alisema zitatoka katika vyanzo mbalimbali vya mapato toka katika miradi ya Halmashauri hiyo, Alitaja baadhi ya vyanzo vya mapato kuwa ni pamoja na vyanzo nya mapato vya ndani ,Ruzuku kutoka serikali kuu na mapato ya mishahara.
Aidha alisema baraza la madiwani lenye wajumbe wapatao 55 wamepitisha bajeti hiyo kwa pamoja .
Kwa upande wake mwenyekiti wa halimashauri hiyo Runyogote Kashunju,alisema kuwa bajeti hiyo huenda ikawa ya mwisho kujadiliwa katika Halmashauri mbili kutokana wilaya ya Kyerwa kujitenga na wilya ya karagwe hivi karibuni.
Aliongeza kuwa kwa mjibu wa kifungu cha 46 ibara ya kwanza kuwa kikao bajeti kitakuwa kinafanyika si chini ya miezi miwili kabla ya kikao cha bunge.
Alisema kwa upande wa bajeti kwa wilaya ya Kyerwa imeidhinishiwa kiasi cha zaid ya shilingi Bilioni 10,na kuongeza kuwa bajeti hizo zitalenga vya ujenzi vya shule za kidato cha tano,Mkile,Bugene na Mabira na ujenzi wa chuo cha ualimu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment