Na,
Mbeki Mbeki
KARAGWE.
Wapiga debe watumishi wa
makanisa, Machinga, Waganga wa kienyeji wamepewa siku 45 kuwa
wameondoka katika miji ya Omrushaka na Kayanga wilayani Karagwe mkoani
Kagera kutokana na kuchangia ongezeko la vitendo vya ujambazi, uvutaji
bangi na ubakaji katika miji hiyo.
Akizungumza katika mikutano ya hadhara jana kwa nyakati tofauti katika
kijiji cha Rukajange na Omrushaka Afisa Mtendaji wa kata ya Bugene
Nestory
Tushabe alisema kuwa katika
miji hiyo kumekuwepo na ongezeko kubwa la vitendo vya ujambazi,
udokozi, ubakaji, uvutaji bhangi vinavyosababishwa na Machinga, baadhi
ya vijana kutoka katika familia mbalimbali, Asekido, wapiga debe,
wahamiaji haramu na baadhi ya watumishi wa makanisa.
Tushabe alisema kuwa katika kipindi Mei hadi Juni mwaka huu zaidi ya
familia kumi katika kata yake zimevamiwa usiku na mali
kadhaa kuporwa ni pamoja
na baadhi ya watu kujeruhiwa katika matukio hayo, ambapo aliongeza kuwa
vijana kumi wamefikishwa mahakamani kutokana na kujihusisha na vitendo
vya ujambazi wa kutumia nguvu kwa nyakati tofauti katika kata hiyo.
Alisema kuwa katika miji hiyo kuna ongezeko kubwa la Wahamiaji haramu
ni pamoja na baadhi ya watumishi wa makanisa ambao pia ni wahamiaji
haramu wanaokuja kwa visingizio vya
kuanzisha makanisa ambapo
nyakati za usiku wanabadilika na kujihusisha na vitendo viovu.
"Inasikitisha kuna wengine nao wanajifanya ni vichaa lakini nyakati za
usiku hawaonekani na hatujui wanaenda wapi na wanalala wapi sasa nasema
hivi sitaki kuona mtu yeyote katika miji hii ambaye hana shughuli yoyote
iliyo halali kwa huruma tu nawapa siku 45 kila mmoja awe ametafuta
mahali pa kwenda" Alisema Tushabe.
Mmoja wa wakazi wa miji hiyo Linus Kishenyi alisema kuwa dolia
iliyofanyika katika kata hiyo kwa vijana 250 walikamatwa kwa siku moja
nyakati za usiku katika katika mazingira ya kutatanisha na kuwa dolia na
ulinzi shirikishi unapaswa wakati wote ili kupunguza vitendo vya
ujambazi vilivyokithiri na kuhatarisha na kuwa na dolia na ulinzi
shirikishi unapaswa wakati wote ili kupunguza vitendo vya ujambazi
vilivyokithiri na kuhatarisha amani katika jamii.
Alisema kuwa kuongezeka kwa ujambazi kunachangiwa na Jeshi la polisi kupelekewa waharifu na kuwaachia kwa muda mfupi, ni pamoja na wenyeji kuwapa makazi wahamiaji haramu kutoka Burundi na Rwanda bila kupeleka taarifa zao kwa wenyeviti wa mitaa na vitongoji.
Naye Diwani wa kata hiyo Alistides Mulilo ambaye pia ndiye aliyekuwa Mwenyekiti wa mkutano huo alisema kuwa tatizo la kukithiri kwa vitendo vya ujambazi linachangiwa na Baa za kupangisha wanakaa na watu bila kujua wanatoka maeneo gani na bila kuwauliza vitambulisho.
Muliro alisema kuwa baadhi ya wazazi wameshindwa kuthibiti tabia za watoto wao na kuwapa uhuru wa kupindukia jambo lililopelekea baadhi ya vijana kujihusisha na vitendo vya uvutaji bangi, madawa ya kulevya na kushindwa kujihusisha na shughuli za ujasiliamali kwa faida ya familia zao na taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake Mkaguzi msaidizi wa Jeshi la polisi wilayani Karagwe Nurdin Tunutu alisema kuwa wananchi wanapaswa kujenga tabia ya kushirikiana na Jeshi la polisi na kutoa taarifa pale wanapobaini kuwa kuna viashiria vya uharifu kwa nyakati zote.
Aidha aliongeza kuwa polisi ni chombo safi, na polisi hawafanyi kazi kwa majungu na kuongeza kuwa raia wamepewa uwezo wa kukamata chini ya kifungu cha 16(9) cha mwaka 1985 kama polisi wanavyoweza kufanya na kuongeza kuwa sheria ya dhamabna wa kupewa dhamana kuwa haoni sababu ya Jeshi la Polisi kupewa lawama pale wanapomwachia mtuhumiwa.

No comments:
Post a Comment