Na
Juhudi Felix
Majita-Musoma Vijijini-Mara
Hii ni moja ya matukio katika picha ambapo timu ya Buhare chuo Cha maendeleo ya Jamii ilipochuana na timu za vijiji viwili huko Musoma vijijini.Timu ya Buhare CDTI ililazimika kugawanyinka katika timu mbili ili kuweza kukithi matakwa ya mamia ya mashabiki wa vijiji hivyo vya Majita.Katika mchezo wa Kwanza timu ya Buhare ambayo ilianza iliweza kushinda kwa goli moja bila ya majibu na katika mchezo wa pili ambao ulizikutanisha timu ya Buhare CDTI na Fagilia SEK mchezo ulioisha kwa matokeo ya sare ya kufungana kwa goli moja kwa moja.Buhare ilijipatia goli la kwanza katika kipindi cha kwanza lakini lilikataliwa kwa madai mfungaji alikuwa ameotea na katika kipindi cha pili buharae walianza mchezo kwa kasi na kupiga pasi za uhakika kiasi cha kuamsha shangwe kwa mashabiki waliofurika katika viwanja hivyo vya shule ya Msingi SEKA iliyoko kijiji cha Majita Musoma Vijijini mkoani Mara.
Fagilia Seka walisawazisha goli hilo dakika tano mchezo kuisha lakini goli hilo lililalamikiwa na mashabiki na viongozi wa timu ya BUHARE CDTI kwani mfungaji wa goli hilo alizuia mpira kwa mkono na kufanikiwa kufunga goli hilo.Mchezo huo uliacha gumzo wa wakazi wa maeneo hayo kutokana na kiwango kilichooneshwa na timu zote mbili.
No comments:
Post a Comment