Meneja wa TRA Morogoro Philip Kamune akimkabidhi mkuu wa magereza ya mahabusu Morogoro Zephania Neligwa baadhi ya dumu za mafuta ya kupikia.
Mamlaka ya mapato Tanzania TRA Mkoa wa Morogoro imekamata dumu zaidi ya 1590 za mafuta ya kupikia ambayo hayajalipiwa usuru wa forodha kodi.
Meneja wa TRA Mkoani Morogoro Philip Kimune amesema dumu hizo hazijalipiwa kodi ya shiling 64.7 hizo zilipitia njia ya Bandari ya Bgamoyo mkoani PWANI.
Alisema baada ya kukamatwa kwa bidhaa hizo na mmiliki wake Said Khalifan kushindwa kulipia kamishina wa forodha TRA makao makuu aliamuru bidhaa hizo zigawiwe kwa taasisi za serikali na makundi maalumu ikiwemo magereza ya mahabusu ya Morogoro na hospitali ya rufaa ya mkoa .

No comments:
Post a Comment