KUSHUKA KWA ELIMU KATIKA MKOA WA KAGERA
NA JUHUD FELIX
01:
UTANGULIZI:
Mkoa wa Kagera upo Magharibi mwa nchi yetu ya Tanzania. Unazo wilaya saba ambazo b Bukoba, Biharamulo, Chato, Karagwe, Missenyi, Muleba na Ngara. Makabila yaliyopo katika mkoa huu ni Wahaya, wanyambo, wahangaza, Wasubi na wasukuma. Mazao ya chakula ni ndizi, mihogo, viazi vitamu, viazi vikuu, maharage na njugu mawe. Mazao ya biashara ni pamoja na
Mkoa wa Kagera upo Magharibi mwa nchi yetu ya Tanzania. Unazo wilaya saba ambazo b Bukoba, Biharamulo, Chato, Karagwe, Missenyi, Muleba na Ngara. Makabila yaliyopo katika mkoa huu ni Wahaya, wanyambo, wahangaza, Wasubi na wasukuma. Mazao ya chakula ni ndizi, mihogo, viazi vitamu, viazi vikuu, maharage na njugu mawe. Mazao ya biashara ni pamoja na
kahawa, pamba na ndizi. Mkoa wa Kagera hupata mvua katika msimu wa vuli na masika.
HALI YA ELIMU
Mkoa
wa Kagera ulikuwa na hali nzuri sana ya kielimu kuanzia miaka ya 1960
hadi mwanzoni mwa miaka ya 1980. Wananchi walikuwa na mwamko mkubwa sana
wa elimu na vijana wengi walijiunga na shule za msingi wachache
waliendelea na elimu ya sekondari katika shule za serikali na wachache
walikwenda kusoma katika shule za sekondari nchini Uganda. Elimu mkani
Kagera ilipewa kipaumbele cha kwanza kwani wanafunzi waliokuwa na tatizo
la upatikani wa mahitaji ya shule walipata msaada toka mfuko wa chama
cha Ushirika na BCU(Buoba Cooperative Union) na hatimaye KCU 1990
LTDkupitia mfuko wa Elimu (Balimi Education Fund) Kutokana na jitihada
za chama cha Ushirika cha Wakulima wa Kahawa (Buni) Kagera wanafunzi
wengi waliendelea na masomo yao hadi chuo kikuu. Wazazi na wananchi kwa
ujumla walihakikisha watoto wote wenye uwezo wa kusoma wanasoma. Vijana
waliohitimu Darasa la Nane, Kidato cha Nne na kuendelea masomo wengi
walifanikiwa kupata ajira hivyo kuboresha maisha yao na familia zao.
Mwanzoni mwa mwaka 1980 Elimu mkoani Kagera ilianza kuorora kutokana na
sababu zifuatazo:-
1. VITA YA KAGERA:
Nchi
yetu iliingia vitani na nchi ya Uganda maarufu kwa VITA YA KAGERA. Vita
hivi vilisababisha watu wengi kupoteza maisha pamoja na mali zao.
Ucchumi wa mkoa na nchi yetu kwa ujumla ulidorora sana na maisha ya
wananchi yalibadilika.
Vita
ilidumu kwa muda mfupi lakini madhara yake yanaonekana hadi leo. Baada
ya vita wanafunzi na watumishi wengi waliacha shule na kazi na kuingia
kenye biashara na walitengeneza fedha nyingi kwa muda mfupi. Vijana
wengi waliona nibora kufanyabiashara badala ya kuendelea na masomo
shuleni. Wafanyakazi nao waliona ni bora kufanyabiasha kulikokuendelea
na kazi za serikali ambazo zilikuwa hazilipi vizuri, kana kwamba hiyo
haitoshi, ugonjwa wa UKIMWI ukaingia katika nchi yetu ukitokea Uganda.
Watu wengi walipoteza maisha bila kujua ni ugonjwa gani ulikuwa
ukiwasumbua. Wanafamilia walitumia muda mwingi kuhudumia wagonjwa badala
ya kufanya kazi za uzalishaji mali ama wanafunzi kwenda shule. Pigo
hilo linaendelea hadi leo. Pesa nyingi zilitumika kuboresha afya badala
ya kulipia karo za wanafunzi.
Aidha watoto wengi wanalazimika kujilea na kulea wadogo zao badala ya kuhudhuria shule.
2. KUSHUKA KWA BEI YA BUNI (KAHAWA)
Suala
linalosababisha kudorora kwa elimu mkoani hapa ni kushuka vibaya kwa
bei ya kahawa katika soko la dunia. Hali hii iliathiri sana uwezo wa
wana Kagera kumudu gharama za masomo kwa watoto wao ndani na nje ya
nchi. Aidha hali hii ilisababisha kuporomoka kwa chama cha KCU 1990 LTD
pamoja na mfuko wa Elimu wa chama hicho uliojulikana kama “Balimi
Education Fund”
3. UKOSEFU WA KAZI AU AJIRA:
Katikati
ya miaka ya 1990 Serikali ilishindwa kuajiri watumishi wapya na
mwishoni mwa miaka hiyo ililazimika kupunguza watumishi wake
(retrenchment) Watumishi waliopunguzwa katika sehemu zao za kazi
walilipwa kiinua mgongo lakini fedha hizo ziliisha ndani ya muda mfupi
na maisha yao yakawa katika hali mbaya. Vijana wengi walihangaika huko
na kule kutafuta ajira bila mafanikio na elimu yao ikaonekana haina
maana yoyote.
4. MATARAJIO YA WAZAZI:
Wazazi
walipokuwa wanatumia rasilimali zao kuwasomesha watoto wao walitazamia
wapate kazi na wawasaidie kuwatunza wazazi wao pamoja na ndugu zao au
familia zao. Baada ya wahitimu kukosa kazi wazazi walikata tamaa na
kuvunjika moyo na hawakuona umuhimu wa kutumika rasilimali zao
kuwasomesha watoto wakati hakuna ajira.
5. UGONJWA WA ZAO LA MIGOMBA
Ugonjwa
wa migomba maarufu kama “Myauko” umeongeza umasikini mkoani Kagera kwa
sababu ni zao la chakula linalopendwa na watu wengi. Wananchi wananunua
ndizi kwa bei kubwa na hivyo kukosa pesa za kuwalipia watoto wao gharama
za kielimu.
6. MWAMKO WA KIELIMU KATIKA MIKOA MINGINE
Tangu
enzi za uhueu wa nchi yetu mikoa iliyokuwa inaongoza kielimu ni
Kilimanjaro, Mbeya na Kagera. Kwa sasa mikoa ambayo ilikuwa imejikita
kwenye ufugaji na biashara za kuni na mkaa imeanza kukimbizana na elimu.
Mkoa wetu upo pembezoni mwa nchi na hamna fursa kama mikoa ya wenzetu.
Hali hii imeufanya mkoa wetu urudi nyuma zaidi kielimu maana ushindani
umekua mkubwa zaidi.
7. JANGA LA MELI YA MV. BUKOBA
Kuzama
kwa Meli ya Mv. Bukoba lilikuwa pigo kubwa kwa mkoa wetu maana walimu
wengi waliopangwa Kagera waligoma kuja kwa kisingizio ch kuogopa kuzama
katika ziwa kwa vile njia ya uhakika wa kuja mkoani Kagera ilikuwa
kupitia ziwa Viktoria mbaya zaidi hata vijana waliozaliwa Kagera baadhi
yao waligoma kuja kufanya kazi hapo. Hali hii imesaidia sana kuishusha
Kagera kielimu.
8. MATUMAINI MAPYA WANAKAGERA
Baada
ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutuunganisha na mikoa
jirani hali ya kielimu imeanza kuboreka Kagera. Mnamo miaka ya 1990
mkoa Kagera ulikuwa unashika nafasi ya kumi na tisa kitaifa, lakini kwa
sasa mkoa wa Kagera ni kati ya mikoa minne bora kielimu nchini.
9. JUKUMU LA MWANAKAGERA
Ni
jukumu letu wana Kagera kuendeleza mkoa wetu kielimu. Elimu ni muhimu
sana kwa watu wetu hata kama hakuna ajira ya kutosha. Hivyo kila mmoja
kwa nafasi yake ajione kuwa anadeni la kuinua kiwango cha elimu. Ipo
haja ya kuitisha mikutao ya hadhara ya kuhamasisha wananchi wafufue ari
ya kuhakikisha watoto na wao wenyewe wanatoa kipaumbele cha kwanza kwa
elimu. Walimu wathaminiwe na wapewe ushirikiano wa kutosha kuitenda
kazi yao.
Kamati
za shule na WDC ziwashawishi wananchi na wazazi kuchangia na
kuindeleza elimu. Irudishwe mifumo ya wanakagera ya kuwasisia wazazi wa
wanafunzi wenye kipato kidogo kwa mikopo yenye masharti nafuu , wale
wote wanaopenda kijiendeleza kielimu. Watafutwe wafadhili wa ndani na
nje ya mkoa wa Kagera wawekeze katika Elimu hapa kwa gharama nafuu hasa
kwa kujenga Vyuo Vikuu. Wanakagera waishio nje ya mkoa huu wawajibike
kufufua umaarifa wa mkoa wao maana mkataa kwao hanatofauti na mtumwa.
No comments:
Post a Comment