Saturday, March 3, 2012

AJIRA KWA WATOTO/UNYANYASAJI WA KIJINSIA

                                           PICHA  KUTOKA  MAKTABA KKKT-KARAGWE  DIOCESE

 NA
       JUHUDI    FELIX-KARAGWE

Wakati  mashirika  na taasisi na wanaharakati kuwa katika harakati za  kupinga ajira kwa watoto ambao wako chini ya umri wa miaka 18 kuajiriwa na kufanyishwa kazi nzito ambazo zinaleta athari katika maendeleo ya makuzi ya watoto hali ni tofauti na wilaya ya Karagwe mkoani Kagera kama picha inavyoonesha  hapo juu.

Mashirika na taasisi zinazotetea unyanyasaji wa kijinsi sijui kama hali hii nao wanaichukuliaje imekuwa ni kawaida wasichana wa umri mdogo kufanyishwa kazi nzito majumbani na kufanyiwa vitendo vya kinyama ambavyo vinadhuru afya zao kimaendeleo pia kiafya  serikali ,wadau na jamii kwa ujumla inabidi kuunganisha jitihada za pamoja katika kupinga ajira kwa watoto.

Hali ya kipato cha wazazi cha kumpeleka mtoto wa kike shule inashindikana kiasi cha kumkatisha tamaa na kumfanya ajiingize kwenye vishawishi vingine na hivyo ili kuondoa tatizo hili katika  jamii yetu ya Kitanzania,kunahitajika jitihada za pamoja za Serikali,Taasisi mbali mbali na wadau wa Maendeleo wawe na dhamira ya kweli na matumizi sahihi za raslimali zilizopo.

Serikali na wadau wa maendeleo na jamii kwa ujumla inabidi kuwabaini watoto wa kike ambao wako katika Mazingira hatarishi kwa sababu ya umaskini wa familia zao wameshindwa kupata haki zao za msingi  kama vile kupata elimu,ushirikishwaji katika mambo yanayowahusu  hivyo na kuamua kujiingiza katika vitendo vya kuajiriwa kwa ajili ya kujipatia kipato cha kukidhi mahitaji yao ya msingi.

No comments:

Post a Comment