Na
JUHUDI FELIX
KARAGWE.
Watu wenye ulemavu wametakiwa kujiunga na vikundi
mbalimbali vya kuweka na kukopa ili kujikwamu na hali duni ya kiuchumi,kuondoa
tabia ya kulalamika na omba omba.
Wito huo ulitolewa na Mkuu wa wilaya ya Karagwe Bi
Dary Ibrahimu Rwegasira wakati akitoa hotuba yake ya
ufunguzi kwenye mdahalo wa kujadili changamoto zinazowakabili watu wenye
ulemavu ulioandaliwa na uongozi wa Chama cha watu wenye ulemavu wa viungo
Chawata mkoa kwa ufadhili wa The Faoundation for civil Society.
Alisema kuwa watu wenye ulemavu wakijiunga kwenye
vikundi vya kuweka na kukuopa yaani vikoba itakuwa ni mkombozi kwao ili
kuondokana na hali ya kuomba omba na kulalamika huku wakiboresha maisha yao.
Bi Rwegasira alisema
kuwa watu wenye ulemavu wakiwa kwenye vikundi ni rahisi kuwasaidia na kujiunga
na huduma mbalimbali za kuwasaidia kupunguza makali ya maisha na ametolea mfano
wa huduma ya Bima ya Afya wakijiunga kwa kuchangia wataweza kutibiwa kwa
gharama nafuu kuliko kulipia kupitia mfumo wa kawaida.
Awali Laurian Pankrasi akisoma risala kwa mgeni rasmi mwenyekiti wa
Chawata mkoa pia katika mradi huu anajulikana kama mratibu amesema kuwa lengo
la mdahalo ni kujadili sera ya maendeleo ya watu wenye ulemavu ya mwaka 2004 na
sheria ya watu wenye ulemavu ya mwaka 2010 kwa ajili ya kuwajengea uwezo watu
wenye ulemavu kujua haki zao za msingi.
Wakichangia mada hiyo wajumbe mbalimbali
waliohudhuria mdahalo huo wamebainisha changamoto mbalimbali zikiwemo
kutoshirikishwa katika nyanja za maamuzi,kupata fursa sawa ya katika
Elimu,ajira, huduma ya Afya,usafiri na kutokuwepo miundo mbinu ambayo si rafiki
kwa watu wenye ulemavu kwenye majengo ya umma.
Changamoto nyingine ni kujinyanyapaa watu wenye
ulemavu wenyewe na kutokuwa na lugha ya usawishi wa kuwasilisha hoja zao kwa
watoa huduma na kuishia kulalamika bila kuweka bidii ya kuwa waadilifu na
urafiki na wanajamii.
Mdahalo huo ambao ulihudhuliwa na watu wenye
ulemavu,viongozi wa taasisi za dini,Viongozi wa Vyama vya siasa,Wanasheria
,madiwani na wataalamu kutoka idara za serikali za ustawi wa jamii,maendeleo ya
jamii,Mipango na idara nyinginezo.
No comments:
Post a Comment