NA
JUHUDI FELIX
KARAGWE
Mamlaka
ya maji safi na taka mjini Karagwe KAUWASA
inakabiliwa na changamoto
mbalimbali ikiwemo uhaba wa vyanzo vya maji vyenye uwezo wa kuhudumia
idadi kubwa ya watu wanaoongezeka kwa kasi katika eneo la mjini na vitongoji vyake.
Hayo
yamesemwa na mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya karagwe Bosco Ndunguru hivi karibuni kwenye kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika kwenye ukumbi wa vijana Angaza mjini kayanga.
Amesema
mamlaka ya maji mjini inakabiliwa na
changamoto mbalimbali ikiwemo uwaba wa vyanzo vya maji
vyenye uwezo wa keweza kuhudumia
idadi kubwa ya watu wanaoongezeka
kwa kasi katika eneo la mjini na
vitongoji vyake jirani.
Changamoto
nyingine ni ufinyu wa fedha za kuendeleza
na kuweza kuwa na vyanzo vya maji vyenye uwezo wa kuzalisha maji ya kutosheleza mahitaji ya mjini,garama
kubwa za uendeshaji kwa upande wa
vipuli vya mitambo na vile vya miundombinu ya mabomba
,ubora wa maji usiokidhi viwango vinavyotakiwa kutokana na kutokuwa na uwezo wa kifedha wa
kujenga mitambo ya kutibu maji nan fedha za inunuzi wa madawa.
Amesema
kuwa.kipindi cha mwaka wa fedha 2012/2013
mamalka ya maji ilikadiria
kukusanya kupitia vyanzo vyake
vya ndani jumla ya shiling
milioni sitini na mbili mia tano tisini na tisa elfu mia tatu sitini na nane na senti ishirini na
tano ambapo amesema hadi January 2013
ilikuwa imekusanya jumla ya shilingi milioni mia nane na thelathini
tano mia tisa thelathini elfu mia saba
sabini na tatu sawa na asilimia
53 .4 ya lengo la mwaka.
Aidha
amesema ofsi yake imeandaa mpango wa ukarabati
wa mradi wa maji kwa chanzo cha charuhanga kwa manufaa ya kutoa huduma ya maji
kwa wakazi wa mij wa Omrushaka na
vijiji vyake jirani.
Hata
hivyo amesema kuwa kuna mambo
kadhaa ambayo yamefanikishwa na
ofsi ya mkurugenzi mtendaji ikiwa ni pamoja na kununuliwa kwa mtambo mpya wa kusukuma maji SP 8A YS kwa chanzo cha maji cha wateja wapya 29 .kuunganisha huduma ya
maji na kufanya jumla ya wateja 413 hadi janualy mwaka huu.
No comments:
Post a Comment