Mahakama
ya wilaya ya Ilala imemuhukumu kifungo
cha cha Maisha
Seleman Nassibu mwenye umri
wa miaka (20) baada
ya kupatikana na
hatia ya kumlawiti
mtoto wa kiume
mwenye umri wa
miaka 13.
Nassibu
ambaye ni mkazi
wa Majohe amehukumiwa
kifungo hicho baada
ya mahakama kujiridhisha
na ushahidi wa
mashahidi wanne uliotolewa mahakamani
hapo.
Akisoma
hukumu hiyo Hakimu
Mkazi Mfawidhi wa
mahakama hiyo Said
Mkasiwa amesema mahakama
imemtia hatiani baada
ya mashitaka kudhibitisha
mashtaka hayo bila
kuacha shaka.
Kabla ya kutoa
adhabu hiyo wakili wa
serikali Eric Shija
aliiomba mahakama kutoa
adhabu kali kwa
mshitakiwa ili iwe
fundisho kwa wengine.
No comments:
Post a Comment