Mfanyabiashara
Andrew Gatawa amehukumiwa
kifungo cha miaka
20 jela baada
ya kupatikana na
hatia ya kuharibu
miundo mbinu ya reli.
Gatawa
amehukumiwa kifungo hicho
katika mahakama ya
Ilala baada ya
kupatikana na hatia
ya kung’oa mataruma
ya reli ambayo
ni mali ya
Mamlaka ya Reli
Tanzania na Zambia
(TAZARA)
Mahakama imewaachia
huru washitakiwa wawili
ambao walikuwemo katika kesi
hiyo kutokana na
upande wa mashitaka
kushindwa kuthibitisha mashtaka
dhidi yao hivyo
kushindwa kuwatia hatiani .
Akisoma
hukumu hiyo Hakimu
Mkazi wa Mahakama
hiyo Flora Mujaya
amewataja washtakiwa walioachiwa
huru na mahakama
kuwa ni Issa
Seif na Abdallah
Hamidu kutokana na
upande wa mashitaka
kushindwa kuthibitisha mashitaka
hivyo kushindwa kuwatia
hatiani.
No comments:
Post a Comment