Wednesday, December 23, 2015

WANANCHI WAITAKA SERIKALI KUMALIZA MGOGORO WA KUTOKUWA NA MWENYEKITI WA KIJIJI.



 
Wananchi  wa    Kijiji  cha  Nyabwegira  wametoa  wito  kwa  uongozi  wa  halmashauri  ya  wilaya  ya  Karagwe  kuhakikisha  wanatafuta  haraka  ufumbuzi  wa  tatizo  la  kutokuwa  na  mwenyekiti  wa  serikali  ya  kijiji   hicho  kwani  unasababisha  shughuli  nyingi  za  maendeleo   zinakwama  kwa  kukosa  uongozi  huo.

 Wametoa  wito  huo  jana    wakiwa  katika  shughuli  za  kujitolea  kwenye   chanzo  cha  maji Kifunjo   kilicho  kwenye  kitongoji  cha  Kilifunjo  B na  A  ambao  waliungana  kufanya  usafi  wa  chanzo  hicho   wakiongozwa  na  Diwani  wa  Kata  hiyo  Edward     Mpaka   wananchi  hao  walisema  kutokuwa  na  mwenyekiti  wa  serikali  ya  kijiji kunasababisha  shughuli  nyingi  za  maendeleo  kukwama    na  kudhoofisha  jitihada  zao




 
Peter   Martine alisema  kutokuwa  na  mwenyekiti  ni  chanzo  cha  matatizo  ya  shughuli  za  maendeleo  kukwama  na  kumtaka  Afisa  Mtendaji  wa  kata  hiyo  David  Itegereize  kulitolea  majibu  kwani aliwahaidi  wananchi  wa  kijiji  hicho  kulitafutia  ufumbuzi  tatizo  hilo  ndani  ya  muda  wa  mwezi  mmoja  lakini  hajawahi  kuwapa  mrejesho.


Naye  Hamdani    Hamada  mkazi  wa  kitongoji  cha  Kilifunjo  A  amesema  kuwa   tatizo  hilo  ni  liinakwamisha  shughuli  nyingi  huku  likitawaliwa  na  itikadi  za  siasa  miongoni  mwao  huku  akimtaka  Afisa  Mtendaji  kulitolea  kauli  na  ambao  wataendelea  kufanya  hivyo  hatua  zichukuliwe.






Diwani  wa  Kata  ya  Ndama   Edward    Mpaka  amesema  anawapongeza  wanbanchi  wa  vitongoji    viwili  vya  Kilifunjoa  A  na  Kilifunjo  B  kujitokeza  kwa  wingi  kufanya  shughuli  za  maendeleo  kwa  kujitolea  na  kuwata  kuendelea  na  moyo  huo  wa  kupenda  maendeleo  na  kufanya  hivyo  kata  hiyo  itasonga  mbele.

Akizungumzia   suala  la kijiji  hicho  kutokuwa  na  mwenyekiti  amesema  wanamtaka  mkurugenzi  kuitisha  uchaguzi  kwa  mujibu  wa  sheria  inavyoeleza  kwani  mwenyekiti  aliyekuwepo  hukumu  ilishatolewa  na  hakukata  rufaa  hivyo  hatakiwi  kuendelea kumiliki  nyaraka  za  serikali  na  inabidi  azikabidhi  mara  moja.

“Tunamtaka  mkurugenzi  mtendaji  wa  halmashauri  ya  Karagwe  wala  hamtumuombi  maana  sheria  inasema  hivyo  aitishe  uchaguzi  ndani  ya  siku 60  sasa  tunamiezi  nane  tangu  hukumu  itolewe  na  aliyekuwa  mwenyekiti  hakukata  rufaa  yoyote  hivyo  nakuagiza  mtendaji mtu  anayemiliki  nyaraka  hizo awe  ameziwasilisha  kwako  kabla  ya  Januari 05  mwakani “Alisema  Mpaka

Aliyekuwa  mwenyekiti  wa  Kijiji  cha  Nyabwegera  Sadick  Athumani  ambaye   katika  uchaguzi  wa  serikali  za  mitaa  alikua  amepita  bila  kupingwa  baada  ya  kumwekea  pingamizi  mshindani  wake  lakini  CHADEMA  walifungua  kesi  mahakamani  na  hukumu  ilitolewa  na  ushindi  huo  ulitenguliwa  na  mahakama  ya  wilaya  ya  Karagwe.

 
Kwa  upande  wake  afisa  Mtendaji  wa  Kata  ya  Ndama  David  Itegereize amesema  kuwa  suala  hilo  la  mwenyekiti  wa  kijiji ameishaliwasilisha  kwenye  ngazi  husika  ili  ziweze  kulifanyia  kazi  hivyo  pindi  atapopewa  majibu  atayawasilisha  kwao  mara  moja.

Aliwataka  watu   wote  wanaofanya  shughuli  za  kibinadamu  kwenye  vyanzo  vya    maji  kwenye  kata  hiyo  kuhakikisha  anasitisha  shughuli  hizo  mara  moja  vinginevyo  utaratibu  wa  sheria    zitatumika  maana  mtu  haruhusiwi  kufanya  shughuli  yoyote  ndani  ya  mita  60  kutoka  kwenye  chanzo  cha  maji.

No comments:

Post a Comment