Chama cha ushirika
wa kuweka na
kukopa cha Karagwe
Vijana Saccoss(KAVISA) kimepata
mafanikio mbalimbali tangu
kuanzishwa kwake mwaka
2013 ikiwemo kuongeza
wanachama pamoja na
kutoa mikopo kwa
vijana iliyosaidia kujikwamua
kimaisha na kujiajiri
na kuondokana na
ukosefu.
Akisoma
taarifa ya bondi
ya chama hicho
mwenyekiti wa ushirika
huo ujulikano kwa
ufupi KAVISA David
Geofrey amesema kuwa
wanachama wameongezeka tangu
kuanzishwa kwake pia
akafafanua kuwa ushirika
huo haufungamani na
upande wowote wa
itikadi za udini,siasa
wala ubaguzi wowote
ule.
Amesema kuwa KAVISA
imefanikiwa kuwaunganisha vijana
na wameweza kutoa
mikopo kwa ambayo
imekuwa chachu ya kuanzisha
miradi mbalimbali ya
kujiajiri huku akibainisha
mafanikio kadhaa ambayo
ni pamoja na
kuongeza wanachama wa
ushirika huo.
Geofrey
amebainisha changamoto zinazokabili
KAVISA kuwa ni
kutokuwa na viongozi
haswa nafasi ya
katibu na mhasibu
na walioajiriwa walishiriki
kukiingiza chama kwenye
hasara kubwa kama
ambavyo hapa amabainisha.
Afisa
maendeleo ya Jamii
wilaya ya Karagwe
Edina Kabyazi ambaye
amekuwa mlezi wa
KAVISA SACOSS amesema
anatamani kuona ushirika
huo ukikua na
kuwa mkubwa na
kusema kuwa ataendelea
kutoa ushirikiano kama
ilivyokuwa mwanzo na
kueleza kuwa sasa
wamempata Afisa Maendeleo
ya Vijana wamtumie
kwa karibu kwani
ndiye mhusika zaidi.
.
Hata hivyo wajumbe
wa mkutano mkuu
wa Karagwe vijana
SACOSS wamempongeza mwenyekiti
kwa kuendelea kuongoza
chama hicho licha
ya kuwa na
mazingira magumu ya
kuendesha ofisi mkutano
huo pia umehudhuriwa
na afisa ushirika
Jones Rweyunge ambaye
naye amekuwa msaada
mkubwa kwa vijana
hao.
No comments:
Post a Comment