Na Mbeki Mbeki
Imebainika kuwa chazo cha ufaulu hafifu kwa wanafunzi wa
shule za msingi na sekondari katika wilaya ya karagwe kinasababishwa na walimu
wengi kukaa mbali na vituo vyao vya kazi.
Kauli hiyo iliyotolewa jana na baadhi ya wadau wa elimu wilayani hapa kuwa wamebaini kuwa asilimia
kubwa ya walimu wanakaa mbali na vituo vyao vya kazi hivyo kushindwa kufundisha
vipindi vyote vya masomo kwa muda unaotakiwa.
Walisema kuwa hali hiyo imesababisha walimu hayo kuchelewa
kuripoti shuleni na kuwahi kuondoka kabla
ya muda wa kazi hivyo kushindwa kufundisha baadhi ya vipindi.
Waliongeza kuwa tatizo hilo
limesababisha wanafunzi wengi kushindwa kufanya vizuri katika mitihani yao na baadhi yao
kuhitimu bila kujua kusoma na kuandika ambapo wanafunzi 59 katika shule
mbalimbali za sekondari wilayani hapa wamebainika hawajui kusoma kuhesabu na
kuandika.
Mmoja wa wadau hao, Anthon Cleophace alisema kuwa kushuka
kwa kiwango cha elimu katika wilaya yao
kunachangiwa na kutokuwa na mwamko wa kuchangia shughuli mbalimbali za elimu.
Alisema kuwa shule nyingi zilizopo pembeni mwa Halmashauri
hiyo kuwa zinahuaba wa nyumba za walimu hali inayochangia uzorotaji wa
ufundishaji kutokana na kuwa na wanafunzi wengi tofauti na idadi ya walimu
waliopo.
Aidha alisema kuwa tabia ya walimu wengi katika wilaya hiyo
kujihusisha na suala la mikopo kumechangia kushusha taaluma katika mashule yao, kuwa walimu
wanashinda mijini kushughulikia mikopo na kutafuta makampuni yanayokopesha na
kuwaacha wanafunzi bila huduma yoyote mashuleni.
No comments:
Post a Comment