Na Mbeki Mbeki
Wananchi mkoani kagera wametakiwa kutojihusisha na vitendo
viovu vinavyochangia kuvuruga amani ndani ya jamii ili weweze kuimalisha
utawala bora nchini
Mkuu wa mkoa wa kagera kanali msitaafu Massawe ameyasema
hayo wakati akifungua mkutano mkuu kati ya wadau wa utawala bora wa mkoa wa
kagera timu ya tathimini ya utawala bora wa Afrika (APRM) katika hotuba
iliyo……….. na katibu tawala wa mkoa wa kagera, Nassoro Mnambila.
Alisema vitendo vya mauaji ya vikongwe na albino ambayo
yanaenda sambamba na imani za ushirikina na tohara wanazofanyiwa wanawake
vinachangia kuangusha sifa mabayo Tanzania inayo ya kuzingatia
masuala ya utawala bora.
Alisema kuwa Tanzania
inazingatia na itahakikisha inaendelea kuzingatia utawala bora ambapo alisema
utawala bora nchini inawapa wananchi nafasi kubwa ya kujadili mambo
yanayowagusa viongozi.
Aidha kanali mstaafu Massawe aliwaomba washiriki wa kikao
hicho kuwakilisha hoja sahihi zinazohusiana na masuala ya utawala nchi ili
kamati ya tathimini iliyoko nchini ili iweze kupata picha halisi.
Naye kiongozi wa timu hiyo profesa Adele Jinadu alisema APRM
ni mpango wa wakuu wan chi za Afrika ulioanzishwa mwaka 2002.
No comments:
Post a Comment