Saturday, June 16, 2012

LUGHA NAYO MUHIMU KUMPUNGUZIA MGONJWA MAUMIVU.

Na:
      Mwandishi wetu
       KARAGWE.                                                                                                                                                 

      Kituo cha Afya, Katani Kayanga Wilayani Karagwe kinakabidhiwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wamadawa, watumishi, na matumizi mabaya ya lugha kwa wagonjwa.

     Kauli hiyo ilitolewa jana na baadhi ya wagonjwa na wahudumu wa wagonjwa katika kituo hicho cha Wilaya kwa nyakati tofauti wakati wakizungumza na waandishi wahabari kituoni hapo.

     Walisema kuwa kituo hicho kinachomilikiwa na Serikali kinakabiriwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa madawa. Watumishi na matumizi mabaya ya lugha kwa wagonjwa na wahudumu wa wagonjwa wanapohitaji msaada wa huduma kutoka kwa wauguzi wa kituo hiki.

     Ambapo waliongeza kuwa mgonjwa anapofika kituoni hapo huambiwa hakuna dawa na                                                   kuagizwa kwenda kununua madawa katika maduka ya madawa na kuwa mara nyingine mgonjwa ukaa kwa muda mrefu bila huduma kwa kisingizio cha kituo kutokuwa na watumishi wakutosha.

     Mmoja wa wahudumu wa wagonjwa Saada khasimu alisema kuwa baadhi ya wauguzi katika kituo hicho wanamatumizi mabaya ya lugha kwa wagonjwa jambo linalokatisha tama kwa wagonjwa, ambapo alisema kuwa baadhi ya wakina mama wanaokuja kujifungua wanaambiwa kujinunulia vifaa.
    
     Katika hatua nyingine Bi, Khasimu alieleza kuwa mazingira ya kituo hicho na mashuka ya wagonjwa kuwa yanakuwa katika hali chafu na kuwa yanaweza kusababisha maambukizi ya magonjwa.

     Pia alisema kuwa kitendo cha kuwachanganya wagonjwa wa kawaida na wale walio katika maambukizi ya virusi vya Ukimwi ni kutowatendea haki kuwa wagonjwa hao walipaswa kupewa jingo lao sawa na mahospitali mengine yanavyofanya.

     Kwa upande wake mganga Mkuu wa Wilaya hiyo. Daktari Eliasi Vicent Mayala amekiri kuwepo kwa hali hiyo ya utendaji mbovu usioridhisha katika kituo hicho na kuwa mkakati wakuboresha utendaji kazi na huduma utakamilika hivi karibuni.

     Aidha Daktari Mayala amesema kuwa sikwamba kituo hicho wameshindwa kujipanga kutoa taarifa za mapungufu yaliyopo katika Ofisi yake jambo ambalo ameahidi kulifanyia utekelezaji mara maja.
   
     Hata hivyo amewataka waganga na wauguzi katika vituo vyote vya Afya katika Wilaya ya Karagwe kufanya kazi yao kwa kufuata kanuni maadili na utaratibu wa kazi yao kuwa atakaebainika kufanya kazi kinyume cha uturatibu Ofisi yake itamchukulia hatua za kinidhamu, na kanuni za utumishi zitafuata.

                                                                                                                                                                           

No comments:

Post a Comment