Na Mwandishi wetu.
Bukoba
MEYA wa Manispaa ya Bukoba Dkt Anatory Amani anadaiwa kumkwida shati na kumfukuza mwandishi wa
habari wa gazeti la Mtanzania ofisini kwake akimtuhumu kuandika habari
za kupotosha kuhusu mradi wa ujenzi wa soko jipya la Bukoba.
Kwa
mujibu wa maelezo yaliyofunguliwa katika kituo cha polisi Bukoba katika
faili namba BU/RB/3161/2012 mlalamikaji ambaye ni Mwandishi wa gazeti
la Mtanzania Audax Mutiganzi anadai tukio hilo lilitokea juzi alasiri
katika ofisi ya kiongozi huyo.
Katika maelezo yake Mutiganzi anadai kuwa alifika katika ofisi za Manispaa akiwa na ofisa mkuu mtendaji wa benki ya posta nchini na Sabasaba Moshingo aliyekuwa kwenye ziara ya siku mbili mkoani Kagera.ambao walikwenda kufanya mazungumzo ya kupatiwa kiwanja cha ujenzi wa ofisi ya benki yao.
Pia katika maelezo yaliyofunguliwa na mwandishi
huyo anadai baada ya kuingia katika ofisi ya Dkt Anatory Amani,kiongozi
huyo ambaye ni Meya wa Manispaa ya Bukoba alimfokea na kumwamuru
kuondoka katika ofisi yake haraka iwezekanavyo.
Mlalamikaji
anadai kuwa Meya huyo alimtuhumu kuandika habari za upotoshaji juu ya
mradi wa ujenzi wa soko jipya na kuwa alimkwida shati,kusukuma nje huku
akibamiza mlango kwa nguvu.
Baadhi
ya viongozi waliotajwa katika maelezo hayo kuwa walishuhudia tukio hilo
ni Ofisa Mkuu Mtendaji wa Benki ya Posta nchini Sabasaba
Moshingo,Meneja wa tawi la Bukoba Maduhu Makoye na Kaimu Mkurugenzi wa
Manispaa hiyo Stephene Nimzihirwa ambapo mtuhumiwa alikwenda kutoa
taarifa kituo cha polisi.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kagera Henry Salewi alitotafutwa ili kujua hatua
zitakazochukuliwa wasaidizi wake walisema hayupo ofisini na hata simu
yake ya mkononi iliita bila kujibiwa.
Pia
mlalamikiwa ambaye ni Meya wa Manispaa Dkt Anatory Aman simu yake
iliita muda mrefu bila kujibiwa pamoja na kutumiwa ujumbe mfupi wa
maneno kuwa waandishi wa walitaka kujua na kusikia upande wa Meya huyo
dhidi ya malalamiko yaliyopo kituo cha polisi ambapo namba ya Meya huyo
ni 0767428607.
Pia
hivi karibuni kupitia barua kumbukumbu namba BMC/120/16/30 ya May
17,2012 iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Hamis Kaputa na
kusambazwa kwenye vyombo vya habari mjini hapa iliwaonya waandishi kuwa wanapotosha taarifa za maamuzi halali ya vikao.
Pia
barua hiyo inawatahadharisha waandishi juu ya kurudiwa mara nyingi kwa
habari zilizodaiwa zimepotoshwa na kuwa Manispaa iko tayari kuchukua
hatua za kisheria kama upotoshaji huo ungeendelea.
"Wasemaji
wa Manispaa ni Mstahiki Meya na Mkurugenzi au atakayekasimiwa madaraka
na sio vinginevyo,ofisi yetu ipo tayari wakati wowote kuwapa waandishi
habari sahihi"inasema sehemu ya barua hiyo.
Manispaa
ya Bukoba ipo mbioni kutekeleza miradi ya ujenzi wa soko jipya,kituo
kipya cha mabasi na upimaji na uuzaji wa viwanja 5,000 miradi
inayotafsriwa kuwa haiwezi kutekelezwa kwa ufanisi kwa wakati mmoja na badala yake itakuwa mzigo kwa Manispaa na wananachi.
No comments:
Post a Comment