Na Mwandishi wetu
Muleba
Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya Muleba wametakiwa kuhakikisha wanatoa mchanganuo kabla ya kwenda
ofisini kwa mhasibu mkuu wa Halmashauri hiyo kuomba pesa ya mafuta
jambo ambalo imedaiwa kuwa itapunguza matumizi mabaya ya fedha ya
Serikali na kuongeza pato la Halmashauri hiyo.
Tamko
hilo limetolewa na mhasibu huyo Everist Shemdoe ambaye ni mgeni katika
Halmashauri hiyo jana wakati wa kikao cha kawaida cha barza la madiwani
cha robo ya tatu ya mwaka kilichopfanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.
“Mimi
na ahidi mbele ya kikao cha baraza la madiwani kuhakikisha sina urafiki
na mtu kuhusu matumizi ya mabaya ya mafuta ya Serikali,nitahitaji
kupewa mchanganuo kwanza yatatumika katika
shughuli gani namba ya gari na mengine ili nijilithishe ndipo nitatoa
kibali cha mtu kuchukua mafuta katika kituo kilichopangwa na sio
vinginevyo siwezi kukukubali mapato ya halmashauri ya kaendelaea kushuka
na kuendelea kushika mkia kati ya halmashauri za
mkoa huu eti kwasababu ya matumizi makubwa katika eneo hili la mafuta
kwani watanzania wa Muleba na Tanzania wanataka kuona pesa yao ya kodi
inakuwa nathamani”alisema Shemdoe.
Alisema
kuwakama watajitahidi kubana mianya ya matumizi ambayo hayana mpangilio
na kuungana kwa pamoja kati ya madiwani na watendaji wakathibiti
kikamilifu matumizi yasiyo ya lazima Halmashauri ya Muleba itapanda na
kukamilisha lengo la makusudio yao.
Alisema
kuwa kamati ya fedha uongozi na mipango ilipitia taarifa ya mapato na
matumizi na kutoa maelekezo kuwa watumishi wote wanaohusika na
ukusanyaji wa mapato wasikae ofisini badala yake wafanye kazi nje (field
work) kwa ajili ya kukusanya mapato.
Alisema
pia kamati hiyo ilipitia taarifa mbalimbali za kila idara na
kujiridhisha juu ya matumizi hayo ambapo kamati hiyo imeendelea
kuwaagiza wakuu wa idara kuzingatia kanuni za fedha wakati wa kufanya
malipo hasa kwa kuzingatia vifungu vilivyoainishwa.
Pia
kamati ilibaini kuwepo kwa madeni mbalimbali ya zabuni ya mialo pamoja
na meza ambapo kwasasa upande wa mialo deni ilikuwa kiasi cha shilingi
milioni 13.8 na deni la meza ni shilingi laki 8.3 ambapo kamati imetoa
maelekezo kwamba madeni yote yakusanywe pale ambapo kuna utata basi
sheria ichukue mkondo wakehata hivyo madeni maengine yale ya nyumba za
watumishi yaliyoonekana kujirudia na maelekezo ni kwamba kama mpangaji /mtumishi hataki kulipa basi aondoke kwenye nyumba za Halmashauri.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa Halmashauri hiyo GeorgeKatomelo alisema kuwa
kwa kipindi cha miezi miwili tangu alipowasili mhasibu mkuu mpya Shemdoe
kutoka katika Halmashauri ya Wilaya ya Moshi vijijini ambapo kwasasa halmashauri ya Muleba imepanda
kwa kiwango cha ukusanyaji mapato ukilinganisha na kipindi cha Januari
mwaka huu Halmashauri hiyo ili kuwa ya Mwisho katika mawasilisho
yaliyowasilishwa katika kikao cha ushauri cha mkoa ambapo ili pata
asilimia 12 ya makusanyo huku Karagwe ikishika nafasi ya kwanza ambayo
ilikusanya asilimia 98 na kwa sasa makusanyo ya Muleba yamepanda kutoka
asilimia 12 hadi asilimia 62 ndani ya miezi miwili ambayo ni sawa na
makusanyo ya shilingi bl.2 ukilinganisha na kiwango walichoamuliwa
kukusanya cha shilingi
bilioni 3.
Naye
diwani wa kata ya Muleba Hassani Milanga aliishauri Halmashauri hiyo
kuhakikisha inatunza na kuzilinda raslimalia za Halamashauri hiyo kwani
ndizo zinazoongeza mapato yanayoiwezesha Halmashauri kusimamma na kuitwa
Halmashauri.
Nao
madiwani kwa nyakati tofauti wametoa tamko kwamba wanawapongeza
watumishi wa Halmashauri hiyo kutokana na kiwango cha ukusanyajiwa
mapato kupanda na kwa muda mfupi huku wakiwashauri kutorudi nuyma bali
wendelee kukaza mwendo ili kuinusuru Halmashauri hiyo ambayo hushika
mkia katika mambo ya maendeleo na ukusanyaji w amapato katika mkoa wa
Kagera.
No comments:
Post a Comment